Jose Mourinho amejibu kauli ya Yaya
Toure aliyedai kuwa meneja huyo wa Chelsea hakuonyesha heshima kwa timu
nyingine za Uingereza kwa kuzungumza wazi kuhusu matumaini yao katika
michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya wiki iliyopita.
Toure ambaye alikuwemo katika kikosi cha Manchester City
kilichopoteza dhidi ya Barcelona siku moja baada ya Arsenal kutolewa na
Bayern Munich,alionekana kutofurahishwa na maneno ya Mourinho lakini
akiongea kuelekea mchezo
wa ligi dhidi ya Aston Villa,alisema kuwa
maneno yake yalikuwa na lengo la kuonyesha ushirikiano pekee.
Huku akisisitiza kuwa,”Kama kusema kabla ya michezo ya Munich na Camp
Nou kuwa michezo hii bado haijaisha kwani Arsenal na Man City wanauwezo
na ubora wa kwenda huko ugenini na kubadilisha mambo,kama kuonyesha
kwangu ushirikiano kwa timu ambazo zinatoka nchi ambayo nafanya kazi
inachukuliwa kama sio heshima,sawa basi hiyo sio heshima.”
0 comments:
Chapisha Maoni