Ijumaa, Machi 14, 2014

AMANDA AKANA KUBAKA ARUSHA

Staa wa sinema za Kibongo, Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ ameanika ukweli juu ya skendo iliyoenea kama moto wa kifuu kuwa amebakwa jijini Arusha.
 Awali, Risasi Jumamosi lilipokea skendo hiyo kutoka kwa vyanzo vyake ambapo ilidaiwa kwamba Amanda alifanyiwa ‘unyambilisi’ huo baada ya kudanganywa kuwa anakwenda kucheza filamu ya ‘madogo’ fulani wa jijini humo.
“Mwanzoni nasikia walihitilafiana kwenye malipo. Amanda alitaka Sh. milioni 2 lakini baadaye walikubaliana laki 8.

“Kweli Amanda alipofika Arusha alipokelewa vizuri na kupelekwa hotelini.
“Nasikia baadaye wale jamaa walimuibukia hotelini wakiwa watatu wakamtisha na kumbaka kisha wakaingia mitini. Kuna kipindi magazeti yaliandika anaumwa,” kilidai chanzo chetu na kuingia mitini.
Baada ya mzigo huo kutua kwenye Dawati la Risasi Jumamosi, Amanda aliwekwa ‘mtu kati’ ndipo akaeleza anachokijua juu ya sakata hilo.
Amanda: “Huo ni uzushi uliotengenezwa na kijana aliyenipigia simu akaniomba nikacheze filamu yake lakini tulishindwa kuelewana.
“Walitaka nikacheze sehemu ya mhusika nkuu kwa laki 4 lakini niliwakatalia nikaawambia wafanye Sh. milioni 2.
“Walilalama sana wakidai ndiyo kwanza wanaanza hivyo wangeomba angalau nicheze vipande vichache. Tulivutana hadi nikafika Sh. laki 8 lakini walishindwa na kudai kuwa najiona niko juu hivyo nitaona.
“Hata kwenye ukurasa wangu wa Facebook, huyo jamaa amekuwa akinichafua. Ukweli ni kwamba sijawahi hata kuonana naye.
“(huku akimpigia simu mama na baba yake) mara yangu ya mwisho kwenda Arusha ilikuwa mwaka 2008. Kama hamuamini muulizeni mama na baba yangu. Sijawahi kubakwa katika maisha yangu.”

0 comments:

Chapisha Maoni