Jumatano, Machi 05, 2014

MOURINHO AKIRI KUWA UBINGWA EPL UKO MIKONONI MWA MANCHESTER CITY


Meneja wa Chelsea,Jose Mourinho ambaye timu yake ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza anahisi kuwa Ubingwa wa ligi kuu hiyo msimu huu upo mikononi mwa Manchester City.

Ushindi wa goli 3-1 dhidi Fulham katika mchezo wa wapinzani wa magharibi ya London siku ya Jumamosi na kipigo cha  Arsenal cha goli 1-0 kutoka kwa Stoke City kilifanya Chelsea kuongoza kwa tofauti ya pointi nne huku Liverpool wakiwa katika nafasi ya pili.
Man City ambao walicheza fainali ya kombe la Capital One siku ya Jumapili dhidi ya Sunderland na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe hilo kwa ushindi wa goli 3-1 wapo katika nafasi ya nne wakiwa wameachwa pointi sita.

0 comments:

Chapisha Maoni