Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa kupambana na ugaidi umeanza leo kwa
kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi na jumuiya mbalimbali za
kimataifa huko Baghdad, mji mkuu wa Iraq. Wathiq al Hashemi Mkuu wa
Kituo cha Kistratijia cha Nahrawayn na ambaye pia ni msemaji wa mkutano
huo amesema kuwa, wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 50 watajadili masuala
mbalimbali yanayohusiana na vitendo vya makundi ya kigaidi. Al Hashemi
amesema kuwa, mkutano huo wa siku mbili unahudhuriwa pia na ujumbe wa
ngazi za juu kutoka nchi mbalimbali za eneo la Mashariki ya Kati,
isipokuwa ujumbe kutoka Saudi Arabia na Qatar. Hivi karibuni Waziri
Mkuu wa Iraq Nouri al Maliki alizitaja nchi nchi hizo mbili kuwa chanzo
cha kushadidi vitendo vya kigaidi nchini humo. Inaelezwa kuwa, makundi
ya wabeba silaha yanayoungwa mkono na nchi hizo mbili, sasa yanaondoka
nchini Syria na kuelekea Iraq kwa minajili ya kuvuruga hali ya usalama
wa taifa hilo la Kiarabu.
0 comments:
Chapisha Maoni