Habari zilizothibitishwa zinaeleza kuwa, sura mbili za mauzo kwenye
sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa
kula kichapo kutoka kwa msanii mwenzao, Adam Kuambiana.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri mchana kweupe
maeneo ya Mikocheni, Dar, hivi karibuni baada ya kuibuka timbwili lenye
ujazo wa kilo kadhaa baina ya mastaa hao.
Kwa mujibu wa chanzo, Wema ndiye
aliyeanza kummwagia Kuambiana maneno ya shombo akimwambia kuwa
ahakikishe siku hiyo haipiti bila kukata kucha za miguuni kwani ni ndefu
na zinatisha.
“Mwanzoni ilikuwa kama utani tu. Wema alimwambia Kuambiana akate kucha, tena itabidi atumie mkasi wa kukatia michongoma maana kwa wembe hazikatiki.
“Mwanzoni ilikuwa kama utani tu. Wema alimwambia Kuambiana akate kucha, tena itabidi atumie mkasi wa kukatia michongoma maana kwa wembe hazikatiki.
“Pia Wema alimwambia yeye hawezi kumwacha mpenzi wake na kucha ndefu kama hizo za Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Ilizidi kudaiwa kwamba wakati Wema akiendelea ‘kumpaka’ Kuambiana, Aunt aliyekuwa amejilaza chini alidakia na kusikika akisema kuwa ni kweli msanii huyo mwenye uwezo wa juu katika fani anatakiwa kukata kucha hizo huku akizungumza
maneno ya shombo kwa jamaa huyo.Ilizidi kudaiwa kwamba wakati Wema akiendelea ‘kumpaka’ Kuambiana, Aunt aliyekuwa amejilaza chini alidakia na kusikika akisema kuwa ni kweli msanii huyo mwenye uwezo wa juu katika fani anatakiwa kukata kucha hizo huku akizungumza
“Baada ya kuona imekuwa ‘too much’,
Kuambiana alipandwa na hasira, akanyanyuka kwenye kochi na kumfuata Wema
kwa lengo la kumpa kipigo,” kilisema chanzo hicho.
Habari zilidai kwamba, Kuambiana alipomfikia Wema alianza kumpiga
vibao hadi meneja wake, Martin Kadinda akaingilia kati kumuokoa
mwanadada huyo ambaye pia ni meneja wake.
Chanzo kilieleza kwamba baada ya kuachana na Wema, msaanii huyo ambaye pia ni ‘dairekta’ wa sinema mbalimbali za Bongo alimfuata Aunt na kuanza kumlamba makofi ya kutosha.
Tukio hilo lilizua tafrani na kuwafanya wasanii wengine waliokuwa eneo hilo wakimbie na kushindwa kuwatetea Aunt na Wema kwa kuogopa kugeuziwa kibao.

Baada ya kuinyaka ishu
hiyo, mapaparazi wetu walimtafuta Kuambiana na kumuuliza kulikoni
kugeuka bondia na kuwapiga warembo hao ambapo alikiri kutokea kwa ishu
huyo.
Alisema kuwa, Wema na Aunt ni kama wadogo zake, tena yeye kama dairekta wao walipaswa kumheshimu na siyo kumvunjia heshima.
Alisema kuwa, Wema na Aunt ni kama wadogo zake, tena yeye kama dairekta wao walipaswa kumheshimu na siyo kumvunjia heshima.
“Akina Wema ni wadogo zangu, wanahitaji kuniheshimu na mimi ndiye
mwongozaji wa filamu yao, kwa nini wanikosee heshima? Hata kama
wamekasirika lakini nimewashikisha adabu,” alisema Kuambiana kwa ile
sauti yake nzito.
Kwa upande wao, walipoulizwa
Aunt na Wema kuhusiana na kichapo walichopewa walisema walishamzoea
jamaa huyo, lakini kwa alilolifanya la kuwapiga makofi aliwakwaza kwa
sababu hata kama ni mwongozaji wa filamu yao lakini alikuwa pale kwa
ajili yao.
Ukiachana na tuki hilo,
Kuambiana anadaiwa kuwa na mkono mwepesi hasa anapokuwa ‘lokesheni’
ambapo mwaka jana, aliwahi kumtia mikononi staa mwingine wa filamu za
Bongo, Rose Ndauka walipokuwa wakirekodi filamu visiwani Zanzibar.
Siku ya tukio hilo, Kuambiana alikuwa akidairekti Filamu ya Distress
in Zanzibar. Alimshutumu Rose kuvaa mavazi tofauti na maagizo yake,
katika kujibishana akamuwasha makofi.
Juni, mwaka jana, Kuambiana alimshushia kipigo Fadhili Joseph ambaye
alimdai fedha za bia alizokunywa kwenye baa yake, Sinza, Dar es Salaam.
Kuambiana aliposhindwa kulipa aliacha laptop (kompyuta mpakato), siku iliyofuata alirudi na kushusha kichapo huku akiitaka laptop hiyo.
Kuambiana aliposhindwa kulipa aliacha laptop (kompyuta mpakato), siku iliyofuata alirudi na kushusha kichapo huku akiitaka laptop hiyo.
Kuambiana alikamatwa na Polisi Kawe, Dar kwa faili la malalamiko
KW/RB/5761/2012 SHAMBULIO. Kesi hiyo ikahamishiwa Kituo cha Polisi
Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa vile ndiyo kituo cha karibu na eneo la tukio.
Mbali na Kuambiana, staa
mwingine ambaye pia ni dairekta wa muvi za Bongo, Issa Musa ‘Cloud’ naye
aliwahi kutoa kipigo cha bakora kwa msanii Blandina Chagula ‘Johari’
kwa kosa la kuchelewa kufika sehemu ya kurekodia filamu.
0 comments:
Chapisha Maoni