Mshiriki wa Miss Kiswahili 2009 Bongo, Rehema Fabian anasumbuliwa na
tatizo la maini na mapafu kuharibika, ugonjwa uliomuua baba’ke.
Akistorisha na mwanahabari wetu, Rehema alifunguka kuwa aliingia
nchini tangu Desemba, mwaka jana, akiwa hoi kiasi cha kufikia kudondoka
kwenye uwanja wa ndege jijini Dar akitokea China alipokuwa akiishi kwa
zaidi ya mwaka.
“Nililazwa kwa zaidi ya wiki mbili katika Hospitali ya Kinondoni
(Dar) kwa Dokta Mvungi. Niligundulika nilikuwa na tatizo kwenye maini na
mapafu ugonjwa uliomuua baba, nashukuru Mungu nimepewa dawa, naendelea
vizuri,” alisema Rehema.
0 comments:
Chapisha Maoni