Habari kubwa wikiendi iliyopita ni madai ya wapendanao Bongo,
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
kuchapana makofi laivu.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyekuwa eneo la tukio, timbwili hilo la
haja lilijiri usiku mnene kwenye studio ya kurekodia nyimbo za Bongo
Fleva za Tanzania House of Talent (THT) ambapo Diamond alikuwa akirekodi
wimbo wa kolabo na msanii wa Kenya, Victoria Kimani ‘Vicky’ na Omary
Faraji ‘Ommy Dimpoz.
Stori ni kwamba wakati wasanii hao watatu wakifanya yao studio, Ommy
alichukua kipande cha video kilichowaonesha wakiwa pamoja huku Diamond
akiwa ‘veri klozi’ na Vicky kisha akakitumbukiza kwenye ukurasa wake wa
mtandao wa kijamii wa Instagram.
Hapo ndipo muvi lilipoanzia kwani ilisemekana kuwa Wema ‘Mama la
Mama’ alikiona kipande hicho cha video ndipo akaunganisha na ule uvumi
wa Diamond ‘kuminya kimalavu’ na Vicky walipokuwa nchini Afrika Kusini
‘Sauz’.
Ilidaiwa kuwa Wema alimtafuta shostito wake kwa sasa, Aunt Ezekiel
ambaye alimuomba ‘amdraivu’ hadi katika studio hizo lakini yeye (Aunt)
hakushuka kwenye gari aina ya Toyota Lexus Harrier la rangi ya pinki.
Mastaa hao wawili ambao wameurudisha uhusiano wao hivi karibuni baada
ya awali kuvunjika, walijikuta kwenye ugomvi mkubwa mara tu Wema
alipozama studio na kukutana na wasanii hao.
Ilidaiwa kuwa Wema alipofika alimhoji Diamond ana uhusiano gani na
Vicky huku akimkumbusha kuwa siku chache zilizopita kulikuwa na tuhuma
za wao kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Ilisemekana kuwa mzozo huo ulianza taratibu lakini baadaye ulikuwa
mkubwa hadi kufikia hatua ya kuchapana makofi huku Ommy na prodyuza
Tuddy Thomas wakifanya kazi kubwa ya kuwaamulia bila mafanikio.
Kwa mujibu wa ‘kronometa’ yetu,
ugomvi huo ulidumu kwa zaidi ya saa mbili huku Diamond akidaiwa
kuichukua simu ya Wema na kuipasua chini.
Ilidaiwa kwamba wakati wawili hao wakipeana ‘nakozi’, kila mmoja alikuwa akimtupia mwenzake lugha ‘mbofumbofu’ kama ‘wewe umetembea na fulani’ huku mwingine akimwambia ‘na wewe mbona umetembea na fulani na fulani na fulani na fulani na fulani na…’.

Ilielezwa kwamba kauli hizo zilimfanya Diamond aishie kumwambia Wema
kuwa yeye ndiye anamuweka mjini kwa sasa hivyo afunge mdomo wake.
Ilidaiwa kuwa Wema alipoendelea na maneno ndipo Diamond akapandwa na hasira hadi akamchania mwanadada huyo dela sehemu ya mgongoni.
Ilidaiwa kuwa Wema alipoendelea na maneno ndipo Diamond akapandwa na hasira hadi akamchania mwanadada huyo dela sehemu ya mgongoni.
“Asikwambie mtu, palichimbika kweli,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya Ommy na Tuddy kufanikiwa kuwaachanisha, Wema alitoka kwa hasira kisha akatimua. Uzuri ni kwamba hakumgusa Vicky.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimsaka Ommy ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo huku akidai ni masuala ya kawaida katika mapenzi.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimsaka Ommy ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo huku akidai ni masuala ya kawaida katika mapenzi.
Kwa upande wake Diamond simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi (SMS) hakujibu.
Alipotafutwa Wema, alieleza ya moyoni juu ya sakata hilo ambapo alisema hayo ni mapenzi na ndiyo raha ya mapenzi.
“Kwenye uhusiano kugombana ndiyo raha yenyewe, mapenzi huwa hayaingiliwi nampenda na nitampenda maisha yote.
“Kwenye uhusiano kugombana ndiyo raha yenyewe, mapenzi huwa hayaingiliwi nampenda na nitampenda maisha yote.
“Kama ni mjinga, taahira ndiyo tayari amekwishakuwa wangu, kumbuka
kuna usemi kuwa chukua jembe ukalime,” alisema staa huyo anayeaminika
kuwa maarufu zaidi kwa sasa Bongo.
Uvumi wa kuwepo kwa uhusiano wa
kimapenzi kati ya Diamond na Vicky ulivuma baada ya wawili hao
kuonekana kwenye picha ya pamoja wakiwa katika One Project Campaign
nchini Afrika Kusini.
Hata hivyo, wote walikana kwa nyakati tofauti.
Hata hivyo, wote walikana kwa nyakati tofauti.
Kuhusu Wema na Diamond
kupigana siyo mara ya kwanza kwani jamaa huyo anayeuza zaidi muziki wa
Bongo Fleva aliwahi kumtoa nundu mrembo huyo enzi za uhusiano wao wa
awali.
0 comments:
Chapisha Maoni