Jumatatu, Machi 17, 2014

BAADA YA VIDIK KUTIMKA MAN U...MACHO YA MOYES YAPO KWA HAWA ILI KUZIBA NAFASI

Beki wa Manchester United,Nemanja Vidic ameuzwa katika klabu ya Inter Milan na anataraji kujiunga na mabingwa hao wa zamani wa Italia mwishoni mwa msimu huku Rio Ferdinand akitaraji kumaliza mkataba wake mwezi Juni.
Hali hiyo inaonyesha wazi kabisa kuwa Manchester United wanapaswa kufanya mabadiliko makubwa sana katika safu ya ulinzi.
Wachezaji kama Phil Jones na Chris Smalling walisajiliwa kuisaidia timu wakati muda ulipofika kwa nyota wenye vipaji kuondoka lakini David Moyes bado anahitaji kuijenga zaidi safu yake ya ulinzi.
Baadhi ya wachezaji wamekuwa wakitajwa na vyombo mbalimbali vya michezo pamoja na wachambuzi wa soka kuwa wanaweza kuwa na nafasi nzuri ya kusajiliwa Old Trafford na kwenda kufanya vizuri katika safu ya ulinzi inayoachwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa.
Thomas Vermaelen
Beki wa Arsenal,Thomas Vermaelen ambaye alichukua unahodha wa klabu hiyo ya Emirates mara baada ya kuondoka kwa Cesc Fabregas lakini ubora wake na nafasi ya kucheza imepungua tangu kuanza kusumbuliwa na majeraha.
Kwasasa amekuwa chaguo la tatu chini ya meneja,Arsene Wenger huku raia huyo wa Belgium akianza michezo mitatu pekee ya ligi kuu ya Uingereza msimu huu.
Vermaelen amecheza michezo 25 katika eneo la beki wa kati tangu kuanza kwa kampeni ya msimu uliopita na alikuwa kipenzi kikubwa cha mashabiki wa Arsenal katika kutengeneza ama kutafuta goli huku akiwa ni mzuri zaidi wa kupandisha mashambulizi na kupiga pasi sahihi zilizokamilika kwa asilimia 86.7% .
Eliaquim Mangala
Nyota huyo wa FC Porto mwenye umri wa miaka 23 anacheza beki wa kati na amekuwa mmoja kati ya walinzi imara na bora barani Ulaya huku akipata nafasi katika timu ya Taifa ya ufaransa.
Pia alionyesha kiwango bora kabisa katika mchezo dhidi ya Uholanzi alipocheza pamoja na beki mwenzake,Raphael Varane huku akiokoa hatari saba na kushinda mipira muhimu 12 na kupiga pasi zilizokamilika kwa asilimia 95%.
Huku baadhi ya vitu akiwa sawa na Vermaelen lakini kufunga kwake magoli mawili na kutengeneza moja anaonekana ni mlinzi hatari zaidi uwanjani.
Davide Astori
Beki huyu amekuwa katika rada ya AC Milan,huku akiwa na umri wa miaka 27 Astori amekuwa muhimili mkubwa katika klabu yake ya Cagliari huku akiitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Italia.
Kufuatia kuitwa na kocha,Cesare Prandelli katika kikosi kitakachokwenda Brazil kwenye Kombe la dunia,beki huyo anaonekana ni bora sana kwasasa huku akiwapa matumaini makubwa nchi yake katika michuano hiyo mikubwa duniani.
Tangu kuanza kwa msimu uliopita,raia huyo wa Italia ameanza michezo 55 akicheza beki wa kati.Ila udhaifu mmoja pekee alionao ni kuruhusu hatari zaidi kutokana na kukosa umakini akiwa alisababisha hatari nne ikiwa ni nyingi zaidi kuliko beki yeyote katika Seria A kwa msimu huo.
Licha ya hivyo bado ni beki mzuri ambaye ana ubora wa kuweza kumrithi Vidic.
Mehdi Benatia
Beki huyu amekuwa katika kiwango bora sana akiwa na klabu ya AS Roma,huku akitengeneza moja ya ulinzi bora sana barani Ulaya msimu huu.
Mehdi Benatia alithibitisha kuwa alitakiwa na baadhi ya timu kubwa msimu uliopita kabla ya kukataa kuondoka Stadio Olimpico.
Roma wanamatumani ya kufuzu kwa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya huku Man United wakionekana kuhaha kupata nafasi hiyo hivyo huenda ikawa ngumu kumpata nyota huyo mwenye umri wa miaka 26.
Raia huyo wa Morocco alianza michezo 45 ya ligi mwenye misimu miwili iliyopita akicheza eneo la beki wa kati huku akionyesha kiwango cha hali ya juu sana.

0 comments:

Chapisha Maoni