Waziri mkuu wa Australia amesema kuwa mitambo ya satelite ya nchi
hiyo imenasa picha za vitu vinavyoonekana kama mabaki ambavyo huenda ni
ya ndege ya Malaysia iliyopotea siku 13 zilizopita.
Waziri mkuu huyo, Tony Abbott, ameliambia bunge mjini Canberra kwamba
picha za satelite zimeonyesha vitu viwili vinavyofanana na mabaki ya
ndege hiyo.
Taarifa hii imejitokeza karibu wiki mbili baada ya ndege hiyo
kutoweka na abiria zaidi ya 200 ikitokea mjini Kuala Lumpur Malaysia
kuelekea Beijing.
Msemaji wa masuala ya usalama wa safari za ndege, John Young, baadaye
alisema kuwa vitu hivyo ambavyo kimoja kina ukubwa wa mita 24,
vim
eonekana umbali wa kilomita 2500 kusini Magharibi mwa pwani ya
Australia.
Aliongeza kwamba, hata hivyo, huenda vitu hivyo si mabaki ya ndege hiyo.
Wakati taarifa hii ilipotolewa, kulikuwa na ndege ya Australia katika
neo hilo , ndege zaidi zinatarajiwa kuwasili katika eneo lenyewe na pia
manowari ya jeshi inaelekea huko.
0 comments:
Chapisha Maoni