Wayne Rooney amekiri kuwa Manchester United imemlipa David Moyes
matokeo mazuri mara baada kupindua matokeo ya kufungwa goli mbili kwenye
mchezo wa kwanza dhidi Olympiakos na kufanikiwa kufuzu kwa robo fainali
ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Robin van Persie alifunga hat-trick wakati Man United akishinda 3-0
katika dimba la Old Trafford na kupunguza kiasi cha presha kwa meneja wa
klabu hiyo.
Moyes amekuwa katika hali tete klabuni hapo kutokana na kuwa na
kipindi cha maumivu ya kutopata matokeo mazuri na timu kuwa kwenye
kiwango kibovu lakini Rooney anaamini ushindi wa mchezo wa pili
umemaanisha Man United wataendelea kupewa nafasi.
0 comments:
Chapisha Maoni