Libya imetishia kushambulia kwa mabomu meli ya Korea Kaskazini iwapo itajaribu kusafirisha mafuta kutoka katika bandari inayodhibitiwa na waasi ya Sidra. Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan amesema, amri imeshatolewa ya kuwatia mbaroni mabaharia wa meli hiyo.
Kabla ya hapo wanamgambo wanaotaka kujitenga walitangaza kuwa wameanza kupakia mafuta katika meli hiyo kwenye bandari ya Sidra, mashariki mwa Libya.
Abb-Rabbo Albarassi, shakshia aliyejitangaza kuwa kiongozi wa harakati ya waasi wanaotaka kujitenga amesema kuwa, serikali ya Zeidani imeshindwa kutekeleza matakwa ya kugawa utajiri wa mafuta, na kwamba wamejaribu kufikia makubaliano na serikali lakini Bunge halikujadili takwa lao.
Waasi wa Libya wameteka bandari kubwa 3 tangu mwezi Agosti huku wakidai kujitenga, suala ambalo limekwamisha uwezo wa serikali wa kuanza tena uuzaji mafuta nje ya nchi.

0 comments:
Chapisha Maoni