Jumanne, Machi 04, 2014

KUNA LOLOTE UNALOLIJUA KUHUSIANA NA JUMATANO YA MAJIVU??? NGOJA NIKUFICHULIE SIRI HII

Leo ni Jumatano ya Majivu. Kwanini Majivu? Kanisa linaendeleza imani ya agano la Kale na Jipya ya kufanya toba. Kama tunavyoona katika kitabu cha Ayubu 42:6.
"Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu na kutubu katika vumbi na majivu "
Hivyo Kanisa linatualika kutafakari mienendo yetu na katika kipindi hiki cha Kwarezma basi na tufanye toba na kumrudia Bwana. Lakini si katika kipindi hiki tu bali katika siku zote za maisha yetu. Matendo makuu matatu inatupasa kuambatana nayo
1. Kusali
2. Kufunga
3. Kutenda mema na kuwajali wasiojiweza

0 comments:

Chapisha Maoni