MSHAMBULIAJI wa Simba kinara wa mabao Ligi Kuu Bara,
Amissi Tambwe, amesema yupo tayari kukaa chini na kufanya mazungumzo na
klabu yoyote inayokubali kazi yake uwanjani, ikiwemo Yanga.
Tambwe, raia wa Burundi ambaye mpaka sasa anaongoza kwa kufumania nyavu mara 19 kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, anazitoa udenda timu nyingi za ligi kutokana na umahiri wake wa kuchungulia nyavu.
Tambwe, raia wa Burundi ambaye mpaka sasa anaongoza kwa kufumania nyavu mara 19 kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, anazitoa udenda timu nyingi za ligi kutokana na umahiri wake wa kuchungulia nyavu.
Tambwe alisema kwamba kama kuna timu inahitaji huduma yake, imsubiri
mpaka amalize mkataba wake Simba unaoisha 2015 au kama wakimtaka kwa
haraka zaidi waufuate uongozi wa Simba na wakiridhiana, yeye yupo tayari
kukaa nao mezani na kuzungamza nao kuhusu maslahi.
Alipoulizwa kama yupo tayari kujiunga na mahasimu wa Simba nchini,
Yanga SC, alisema kuwa mpira ndiyo kazi yake, hivyo atacheza popote
ilimradi kuna maslahi.
“Nitacheza popote kwa kuwa mpira ndiyo kazi yangu, timu itabaki kuwa timu na mimi ni mchezaji nitabaki kuwa mchezaji ambaye leo nipo huku kesho nipo kule na kama timu ikinitaka mimi bado ni mali ya Simba, ikazungumze na uongozi kwanza.

“Mimi sitakuwa na shida yoyote kama uongozi utaniambia umekubaliana
kuhusu mimi kuondoka, lakini pia kama mkataba wangu na Simba utakuwa
umekwisha nitakuwa tayari kuzungumza na yeyote hata kama ni hao Yanga.,”
alisema Tambwe huku akionyesha kujiamini.
Tambwe aliwahi kusema kuwa Yanga ilikuwa inamtaka awali kabla hajajiunga na Simba akitokea Vital’ O ya Burundi.
Hata hivyo kwa sasa itakuwa vigumu Simba kumruhusu kuzungumza na
klabu nyingine kwa kuwa ndiye amekuwa mkombozi wao kwenye ligi kuu.

0 comments:
Chapisha Maoni