MSANII wa filamu za Kibongo, Kimlola Kimlola ‘Nelly Kim’ amesema
anajivunia sana kufanya sinema nyingi na marehemu Steven Kanumba na
kwamba amejipanga kufuata nyayo zake ili aweze kufanikiwa kwa kutumia
kipaji chake.
Akizungumza na Fichuo, Nelly Kim alisema: “Nafurahi kufanya kazi
na marehemu Kanumba. Nimecheza naye zaidi ya sinema 20 pale kwa Mtitu
Game.
Nimejifunza kujiongoza na kuamini katika mambo makubwa, ndiyo maana
sasa hivi nasimama na kampuni yangu ya Kasinge Production ambayo
inatayarisha na kusambaza filamu.
“Nimesharekodi filamu ya kwanza inayoitwa The Word of God ambayo nimecheza na Kajala, Ben, Kambi na wengineo.
Unajua wasanii hatujitambui, tunakubali kunyonywa wakati tunaweza
kujitutumua na kusimamia kazi zetu wenyewe. Hiyo ndiyo siri ya mafanikio
ya Kanumba ambayo nataka kuitumia ili kufaidika kwenye sanaa.”





0 comments:
Chapisha Maoni