Uwasilishwaji wa rasimu ya katiba uliokuwa ufanywe na mwenyekiti wa
tume ya mabadiliko ya katiba Mh jaji Joseph Warioba umeshindwa
kufanyika baada ya baadhi ya wajumbe ambao ni wanachama wa umoja wa
katiba ya wananchi kusimama na kuanza kuzomea ,kupiga makofi na
kuzungumza bila ya utaratibu wa kipinga kuwasilishwa kwa rasimu hiyo kwa
kile walichodai kuwa kanuni zimekiukwa.
Siyo kwamba ni sokoni bali ni wajumbe wa bunge
maaalum la katiba ambao wanapinga kuwasilshwa kwa rasimu hiyo ambapo
licha ya mwenyekiti wa bunge hilo Mh Samweli Sitta kumtaka jaji
Warioba kuendelea haikuwezekana.
Baada ya hali hiyo tulizungumza na wabunge
ambao wanaunga mkono kitendo kilichofanyika cha kuzuia kuwasilishwa kwa
rasimu hiyo ambapo walikilaani vikali.
Aidha kwa upande wa wabunge ambao wanaunga mkono
kilichotokea bungeni wamesema mwenyekiti ameanza kwa kukiuka kanuni
kana kwamba wakati zinapitishwa hakuwepo na hivyo hawawezi kamwe
kukubali kuburuzwa.
Hata hivyo licha ya kusitishwa kwa bunge hilo
wajumbe waliendelea kukaa ndani ya ukumbi huo wakipiga soga hatua
mbayop ilipelekea kutolewa kwa tango lingine la kuwataka watoke nje.
0 comments:
Chapisha Maoni