Kipindi cha Kwarezma ni kipindi cha Toba na kumrudia Mungu. Tunafunga na kusali katika siku arobaini tukiomba msamaha na kutenda mema. Injili inatuambia Kristu pia alifunga siku arobaini. Kama Yesu hakuhitaji kufanya toba kwa maana hakua na doa la dhambi, kwanini basi ikampasa kufunga? Yawezekana zaidi ya toba mafungo humaanisha kitu kingine pia?
Tukumbuke baada tu ya kubatizwa Kristu alikwenda peke yake jangwani kufanya mafungo. Hii ilikua ni kabla ya kuanza kazi ya kuhubiri Neno la Mungu Israel nzima. Hivyo alihitaji ukaribu na Mungu akiomba nguvu awezeshwe kutimiza aliyotumwa na Baba. Ukaribu huu akauambatanisha na mafungo na sala. Mahala pengine tunamwona Musa aliyefunga kwa siku arobaini kabla ya kupokea Amri kumi za Mungu pale mlimani Sinai (Kutoka 34:28). Hivyo basi Mungu anapotuagiza kumtumikia twahitaji kuwa karibu naye na kumuita katika sala na mafungo.
Lakini tukiwa katika hali hiyo ya ukaribu na Mungu, Yule mwovu shetani hapendezewi. Atafuta kila hila kuharibu safari hiyo ya sala. Hivyo Injili ya Dominika hii inazungumzia majadiliano kati ya Kristu na shetani katika hila zake za kumjaribu Kristu na kumtoa katika ukaribu wake na Mungu ili ashindwe kutekeleza yale aliyotumwa na Baba. Katika kumjibu na kumshinda shetani, Kristu anatufundisha umuhimu wa kufahamu neno la Mungu yaani Biblia. Anatumia Neno la Mungu kama siraha yake ya ushindi. Kila jaribu analotupa shetani Kristu analijibu kwa kusema…”Imeeandikwa katika Maandiko Matakatifu….” (Mathayo 4:4)
Hivyo basi katika safari yetu hii ya kwarezma, ni vyema tukumbuke kuwa mwovu anaranda randa akitafuta nafasi ya kutulaghai ili tudondoke. Tusali, tufaye mafungo na tulifahamu na kulitafakari “Andiko Takatafu” la Mungu
Hivyo basi katika safari yetu hii ya kwarezma, ni vyema tukumbuke kuwa mwovu anaranda randa akitafuta nafasi ya kutulaghai ili tudondoke. Tusali, tufaye mafungo na tulifahamu na kulitafakari “Andiko Takatafu” la Mungu
0 comments:
Chapisha Maoni