WIMBI la wasanii kuingia kwenye siasa limeendelea kushika kasi ambapo
awamu hii msanii wa maigizo na filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’
ametangaza kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
‘Akistorisha’ na paparazi wetu, Dude alisema kutokana na sanaa
kutotoa masilahi ipasavyo, ameamua kuingia kwenye ulingo wa siasa ambapo
anatarajia ‘kunyakua’ Jimbo la Tabora Mjini ambalo kwa sasa linaongozwa
na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage.
“Natarajia kugombea ubunge nyumbani kwetu Tabora mjini, niko tayari
kuchuana na Rage na kwa sasa nipo katika maandalizi ikiwemo kuwa karibu
na wananchi kwani wananikubali sana, hivyo natarajia ushindi tu,”
alisema Dude.
0 comments:
Chapisha Maoni