NI mwaka mmoja tangu alipofiwa na mumewe, Said
Juma Kilowoko ‘Sajuki’, staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amesema sasa
yupo tayari kuolewa lakini sharti la kwanza la muoaji lazima awe mtu
mwenye fedha zake.
Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Fichuo Tz kwa njia ya simu,Wastara amesema kuwa amekuwa mpweke kwa muda mrefu na sasa ni wakati
muafaka wa kumpata mtu wa kuziba pengo la marehemu mume wake.
“Inatosha
sasa, nadhani muda wa kuwa na mwenzangu umefika. Napenda huyo mwanaume
awe mwenye huruma, upendo na kutambua thamani ya mke lakini ni vizuri
akiwa mwenye kujituma na awe na fedha nyingi.
“Natamani kuolewa na bilionea. Najua nikiwa na mwanaume wa aina hiyo
sitateseka, nitapata kila ninachokitaka. Unajua mimi kama mwanamke nina
mambo mengi. Siyo siri natamani itokee siku moja niendeshe Hummer au
Prado (aina za magari) kulingana na hadhi yangu.
“Kiukweli nitafurahi sana nikimpata mwanaume wa aina hiyo, maana
nitakuwa na uhakika wa kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kunisaidia
katika shughuli zangu za sanaa,” alisema Wastara.
0 comments:
Chapisha Maoni