Viongozi wa upinzani nchini Ukraine wametoa muda wa masaa 24 kwa Rais Viktor Yanukovych kujiuzulu baada ya mazungumzo kushindwa kutatua mkwamo wa kisiasa wa nchi hiyo.
Kiongozi wa upinzani Vitali Klitschko amewaambia makumi ya maelfu ya wapinzani katika mji mkuu Kiev kwamba Rais Yanukovych anaweza kusaidia jitihada za kutatua mgogoro huo bila umwagaji damu kwa kuitisha uchaguzi wa mapema.
Ameongeza kuwa iwapo hatafanya hivyo au kujiuzulu basi hii leo ataongoza waandamanaji wa upinzani kufanya mashambulizi katika mji wa Kiev.
Waziri Mkuu wa Ukraine Mykola Azavor amesema, kuna uwezekano wa kufikiwa makubaliano lakini upinzani haupaswi kutainisha muda kwa serikali. Hayo yanajiri huku watu wawili wakiuawa katika ghasia zilizotokea jana kati ya waandamanaji na vikosi vya polisi mjini Kiev.
Nchi ya Ukraine imetumbukia katika machafuko tangu Rais Yanukovych alipokataa kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya na badala yake kujikurubishwa kwa Russia.
Nchi ya Ukraine imetumbukia katika machafuko tangu Rais Yanukovych alipokataa kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya na badala yake kujikurubishwa kwa Russia.




0 comments:
Chapisha Maoni