kuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro aikataa taarifa ya matumizi
ya fedha zaidi ya Sh174 milioni za miradi miwili ya bwawa la maji katika
Kijiji cha Iyula na Msia wilayani hapa na kutoa wiki moja kwa
halmashauri ya wilaya kutoa maelezo sahihi ya miradi hiyo.
Katika fedha hizo,Sh134 milioni zimetumika katika
Mradi wa Bwawa la Maji katika Kijiji cha Iyula huku fedha zilizopokelewa
kutoka serikalini zikiwa Sh250 milioni na nyingine ni Sh40 milioni za
Mradi wa Bwawa la Kijiji cha Msia ambapo fedha hizo zimetumika huku
mradi ukiwa bado haujaanza kutekelezwa.
Alipotembelea miradi hiyo, Kandoro alisema, katika
Mradi wa Bwawa la Iyula taarifa ya mkaguzi inaonyesha, fedha
zilizopokelewa ni Sh250 milioni na zilizotumika ni Sh134 milioni. “Fedha
zingine zimekwenda wapi kwani akaunti ya kijiji zilitolewa fedha zote
Sh250 milioni na mbaya zaidi mmeomba fedha zingine nahitaji maelezo
sikubaliani na taarifa yenu,”alisema Kandoro.
Kuhusu mradi wa Bwawa la Msia, Kandoro alisema
hakubaliani na taarifa ya matumizi ya fedha hizo ambazo ni Sh40 milioni
kwani hakuna kazi iliyofanyika zaidi ya michoro, utafiti na semina.
Alisema Serikali ya mkoa haiwezi kukubali kuona
fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi zinatumika vibaya na yeyote
atakaye bainika kuhusika na ubadhilifu wa fedha hizo, ikiwa ni pamoja na
kubadilisha matumizi yaliyokusudiwa atachukuliwa hatua kali za
kisheria.
“Fedha nyingi za Serikali zinaletwa huku lakini hazitumiki kama ilivyokusudiwa,”alisema
Mwenyekiti wa Kamati ya Mradi wa Bwawa la Iyula,
Jua Mwamlima alisema, walipokea fedha katika akaunti ya kijiji Sh250
milioni na fedha hizo zilitolewa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza
zilitolewa Sh115 milioni na awamu ya pili zilitolewa Sh134 milioni.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mradi wa Bwawa la
Msia,Godwell alisema kuwa,fedha hizo walizitumia kwa ajili ya
semina,kuwalipa waliofanya utafiti na wataalamu wa michoro .
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi,Dk Michael Kadeghe alisema atahakikisha anasimamia maagizo hayo.



0 comments:
Chapisha Maoni