Serikali ya Sudan Kusini na waasi nchini humo wametia saini
makubaliano ya kusitisha mapigano katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis
Ababa.
Machafuko ya ndani nchini Sudan Kusini yamesababisha vifo vya maelfu ya watu katika nchi hiyo changa zaidi duniani.
Wawakilishi wa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na kiongozi wa waasi
Riek Machar walitia saini makubaliano hayo jana chini ya upatanishi wa
jumuiya ya IGAD. Makubaliano hayo yanasisitiza kuwa mapigano nchini
Sudan Kusini yanapaswa kusitishwa katika kipindi cha masaa 24.
Wapatanishi katika mzozo huo wamesema makubaliano hayo yataweka
utaratibu wa kusimamia usitisha mapigano na kuruhusiwa shughuli za
wafanyakazi wa operesheni za misaada ya kibinadamu.
Mapigano ya ndani nchini Sudan Kusini kati ya jeshi la serikali na
waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa rais Riek Machar yalianza
tarehe 15 Disemba mwaka 2013. Baadaye mapigano hayo yalichukua sura ya
kikabila baina ya kabila la Dinka la Rais Kiir na lile na Noer na
Machar.




0 comments:
Chapisha Maoni