Siku kama ya leo miaka 221 iliyopita Mfalme Louis XIV wa Ufaransa
alinyongwa. Alichukua hatamu za uongozi mwaka 1774 na kuathiriwa mno na
mkewe Marie-Antoinette. Mwaka 1789 wananchi wa Ufaransa walianzisha
mapambano dhidi ya Mfalme Louis XIV kutokana na hali mbaya ya kiuchumi
na kijamii na miaka mitatu baadaye serikali ya kifalme ilifutwa rasmi
nchini Ufaransa. Hata hivyo kutokana na kuwa Mfalme Louis alikuwa
ameomba msaada wa nchi za kigeni kwa siri alituhumiwa kuwa amefanya
uhaini na kuhukukiwa kifo. Watu kadhaa wa familia ya Mfalme Louis XIV
akiwemo mkewe Marie-Antoinette pia walinyongwa.
0 comments:
Chapisha Maoni