MNAMO
TAREHE 20.01.2014 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA –TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. DAINA D/O KIHABA,
MIAKA 80, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA SYUKULA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA
MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU
ALIJERUHIWA KWA KUKATWA PANGA KICHWANI NA MIKONONI TAREHE 19.01.2014 MAJIRA YA SAA
21:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA SYUKULA,
KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE NA HOSEA S/O MWAISWELO, MIAKA 20, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA
SYUKULA. CHANZO KINACHUNGUZWA HATA HIVYO
UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA MTUHUMIWA ANA MATATIZO YA AKILI. MBINU NI
KUMVAMIA MAREHEMU AKIWA NDANI YA NYUMBA
ANAKULA CHAKULA NA MJUKUU WAKE ESTER D/O KITWIKA, MIAKA 9, KYUSA,
MWANAFUNZI S/MSINGI SYUKULA STD IV AMBAYE ALIJERUHIWA NA KUPATIWA MATIBABU
KISHA KURUHUSIWA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII PALE WANAPOKUWA NA MGONJWA/WAGONJWA WA
AKILI NI VIZURI KUHAKIKISHA ANAPELEKWA HOSPITALI KUPATIWA TIBA ILI KUEPUSHA
MADHARA YA AINA YOYOTE KWAKE NA KWA JAMII NZIMA.
WILAYA YA MBEYA MJINI –
AJALI YA MOTO.
MNAMO
TAREHE 21.01.2014 MAJIRA YA SAA 01:00HRS HUKO ENEO LA MWANJELWA, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA
JIJI NA MKOA WA MBEYA. MFIKEMO S/O OSIA,
MIAKA 50, KYUSA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA BLOCK Q ALIGUNDUA KUUNGUA MOTO KWA
VYUMBA VIWILI VYA MADUKA YA NGUO MALI
YA WAPANGAJI WAKE WAWILI WALIOFAHAMIKA
KWA JINA MOJA MOJA VICK D/O ? NA MELELE S/O ?
NA KUSABABISHA MALI YOTE KUTEKETEA. DUKA HILO LINA JUMLA YA VYUMBA VITANO.
CHANZO BADO KUFAHAMIKA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA HAIJAFAHAMIKA.
HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU
YALIYOTOKEA. MOTO HUO ULIZIMWA NA KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA
KUSHIRIKIANA NA POLISI NA WANANCHI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI KWA KUCHUKUA TAHADHARI YA MAJANGA
YA MOTO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI
– AJALI YA UPEPO.
MNAMO TAREHE 20.01.2014 MAJIRA YA SAA
13:00HRS HUKO KATIKA VITONGOJI VYA MLIMA RELI, CHAPAKAZI NA MTAKUJA
VILIVYOPO KATA YA UTENGULE USONGWE, TARAFA YA BONDE LA SONGWE, WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. UPEPO MKALI [KIMBUNGA] ULIOAMBATANA NA
MVUA ULISABABISHA ATHARI KUBWA KWA KUEZUA MAPAA YA NYUMBA 15 ZA KUISHI WATU, VIBANDA VYA BIASHARA 18 NA KANISA MOJA EAGT.
HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYOTOKEA. THAMANI HALISI YA UHARIBIFU BADO
KUFAHAMIKA IKIWA NI PAMOJA NA IDADI KAMILI YA FAMILIA ZILIZOATHIRIKA. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Signed
by:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni