Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria
Walid al Moallim amekosoa hatua ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki-moon ya kutengua mwaliko wake kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa
kushiriki katika mkutano wa Geneva II na kukitaja kitendo hicho kuwa ni
kichekesho.
Walid al Moallim ameashiria mchango mkubwa wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran katika kuimarisha amani na usalama wa Mashariki ya Kati
na kusema kuwa, si rahisi kupuuza nafasi ya Iran katika masuala ya
usalama wa eneo hilo na kwamba ni kosa kubwa kutoalikwa Tehran katika
mkutano wa Geneva 2.
Amesema kuwa nchi ambazo hazitaki Iran ishiriki
kwenye mkutano huo kwa hakika zinataka kuendelea hali ya sasa nchini
Syria.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema
mwaliko wa Umoja wa Mataifa kwa Iran kushiriki mkutano wa Geneva 2 na
baadaye kutenguliwa mwaliko huo ni fedheha ya kisiasa kwa taasisi hiyo
ya kimataifa.
Mkutano wa Geneva II unaojadili suala la kukomesha mgogoro wa Syria umepangwa kuanza leo katika mji wa Montreux nchini Uswisi.
0 comments:
Chapisha Maoni