Bunge la Somalia limepasisha kwa
sauti nyingi serikali mpya iliyoundwa Ijumaa iliyopita na Waziri Mkuu wa
nchi hiyo Abdiweli Sheikh Ahmed. Bunge hilo pia ambalo lilikutana jana
mjini Mogadishu lilipasisha mipango ya serikali mpya ya Somalia katika
kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Wabunge hao walijadili siasa za serikali
ya Abdiweli Sheikh Ahmed ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusiana na
usalama, uchumi, kuanzisha taasisi mpya za serikali na kukomboa maeneo
ambayo yangali yanadhibitiwa na wapiganaji wa kundi la al Shabab.
Serikali iliyopasishwa jana na Bunge
nchini Somalia ni ya pili baada ya kumalizika kipindi cha mpito Agosti
mwaka 2012. Mwezi Disemba mwaka jana Bunge la Somalia liliiuzulu
serikali ya zamani ya nchi hiyo kwa tuhuma za kushindwa kutekeleza
majukumu yake na hitilafu kali zilizokuwepo kati ya Waziri Mkuu na Rais
wa nchi.
Serikali mpya ya Somalia itakuwa na
jukumu la kutayarisha mazingira mazuri ya uchaguzi mkuu uliopangwa
kufanyika mwaka 2016 na kushughulikia masuala mbalimbali ya ndani.



0 comments:
Chapisha Maoni