Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania na mkali wa muziki wa R&B Benard Paul maarufu kama Ben Pol amefunguka juu ya hofu iliyotanda kwa watu mashuhuri nchini Tanzania baada ya utabiri wa mtoto wa aliyekuwa mtabiri maarufu hapa Bongo Sheikh Yahaya, Maalim Hussein.
Mwanzoni kabisa mwa mwaka huu Maalim Hussein alitabiri kuwa kwa kuwa mwaka 2014 ulianzia siku ya jumatano basi ni mwaka wa hatari na majanga na ni mwaka wa vifo kwa wasanii na wanahabari.
Fichuo Tz tumeongea na Ben Pol ambaye pia ni mmoja kati ya wasanii waliopatwa na hofu ya maisha yao baada ya kusikia utabiri huo,“Tukazane kumuomba Mungu kwa njia yoyote ile tutashinda hili jaribu." Alisema Ben Pol ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake 'waubani' alioumba na Alice.

0 comments:
Chapisha Maoni