Mchezaji mashuhuri za zamani wa mpira wa vikapu
nchini Marekani Dennis Rodman ameteta vikali ziara yake ya Korea
Kaskazini kabla ya mechi maalum ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais
wa nchi hiyo Kim Jong-un.
Rais Kim Jong-un akiwa na Dennis Rodman |
Katika mahojiano na shirika la habari la CNN,
alihojiwa kuhusu ikiwa atazungumzia swala la mfungwa wa Marekani aliye
kizuizini nchini humo.
Dennis Rodman enzi za ujana wake |
Ziara ya Rodman, imekosolewa na mashirika ya
kutetea haki za binadamu, huku Marekani ikisema kuwa Rodman hawakilishi
Marekani katika ziara yake.
Wachezaji wa iliyokuwa timu yake ya zamani ya
NBA watamenyana na timu ya Korea Kaskazini katika mechi ya maonyesho
siku ya Jumatano mjini Pyongyang.
Rodman anasema kuwa mechi hiyo ni ya
kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Rais Kim Jong-un, ingawa siku rasmi ya
kuzaliwa kwake pamoja na umri wake haijatangazwa rasmi.
Aidha ziara ya Rodman inakuja wiki chache baada
ya kuuawa kwa mjombake Kim , Chang Song-thaek, ambaye wakati mmoja
alioenekana kama mtu shupavu.
Kuuawa kwake kulizua wasiwasi kuhusu uthabiti wa nchi hiyo.
Wakati huohuo, uchaguzi wa wabunge nchini humo
utafanyika tarehe 9 mwezi Machi. Wadadisi wanasema uchaguzi huo utatoa
ishara ya nani wanasiasa wenye ushawishi mkubwa hasa baada ya Bwana
Chang kuuawa.
0 comments:
Chapisha Maoni