Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema leo kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Kenya ili kulinda maslahi ya nchi mbili hizo.
Akihutubia Kongamano la Magavana wa Kenya katika mji wa Naivasha,
Rais Kagame wa Rwanda amesema viongozi wa Afrika wanaweza kutatua
matatizo yanayowakabili wananchi wao iwapo watawashirikisha katika hatua
za kuchukua maamuzi badala ya kuchukua maamuzi ya upande mmoja. Rais
Kagame ambaye alikuwa mgeni wa heshima kwenye kongamano hilo
amewapongeza Wakenya kwa kukubali mfumo wa serikali za majimbo akisema
ni kupitia mfumo kama huo ndipo huduma zinaweza kuwafikia kwa haraka.
Amesema Rwanda imeona manufaa ya mfumo wa majimbo na angependa kuona
hatua za maendeleo zinazoonekana nchini mwake ziweze pia kushuhudiwa
nchini Kenya.
Hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta imesomwa kwa niaba yake na Waziri wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Dkt. Fred Matiangi ambaye amesema
serikali ina azma na irada thabiti ya kuona mfumo wa ugatuzi
unafanikiwa.
0 comments:
Chapisha Maoni