Siku moja baada ya serikali ya Tanzania kutangaza baraza Jipya la
Mawaziri, wadau mbalimbali nchini humo wametoa maoni yao kuhusiana na
baraza hilo.
Kambi ya upinzani hususan Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kimekosoa baraza hilo jipya kikisema Rais Jakaya Kikwete amewachezea
shere Watanzania kwa kuwaondoa mawaziri wachapakazi na kuwabakisha wale
wanaodaiwa kuwa ‘mzigo’. Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbrod Slaa
amesema baraza jipya la mawaziri linaashiria kushindwa Rais Kikwete
kuelewa mahitaji ya Watanzania.
Wasomi kwa upande wao wamekosoa hatua ya Rais Kikwete ya kumbakisha
Waziri wa Elimu, Shukuru Kawambwa, wakisema mwanasiasa huyo ameiletea
Tanzania aibu kubwa baada ya wizara yake kukumbwa na kashfa mbalimbali
katika miaka ya hivi karibuni. Baadhi ya mawaziri wamehamishwa kutoka
wizara moja hadi nyengine huku baadhi ya manaibu mawaziri wakipandishwa
vyeo na kuwa mawaziri kamili na mawaziri wengine wakipigwa kalamu
nyekundu.
0 comments:
Chapisha Maoni