Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, mh Jakaya Mrisho Kikwete amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na naibu Mawaziri katika wizara mbali mbali nchini Tanzania huku wizara nyingine kuachwa bila kufanyiwa marekebisho.
Katika ofisi ya makamu wa rais mh mhandisi, Binilith Satano (Mb) ameteuliwa kuwa Waziri wa nchi Mazingira, wizara ya fedha wameteuliwa mh. Saada Mkuya Salum(mb)ambaye sasa ni waziri wa Fedha,.
Katika ofisi ya makamu wa rais mh mhandisi, Binilith Satano (Mb) ameteuliwa kuwa Waziri wa nchi Mazingira, wizara ya fedha wameteuliwa mh. Saada Mkuya Salum(mb)ambaye sasa ni waziri wa Fedha,.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi7knRWYSZLa2z_jy3acDxRDmtklM4G2cp94e6eKZPDUYoCyCrQT6zmHYjinsxyiITPcEP4MLyq9GxINYt2WmxN4k8q1SCMDWoYxi76hK6J6kFpU7AaecAioQG2mGt0zsxEY5IqNSLIdU3p/s1600/800px-Dar_Ikulu-tz.jpg)
Na manaibu waziri walioteuliwa kufuatia uteuzi huo ni Mh. Mwigulu Lameck Nchemba(mb)amekuwa naibu waziri wa fedha , Mh. Adam Kighoma Ali Malima (mb) pia ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa fedha, Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb) Naibu Waziri ofisi ya makamu wa rais, Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb) Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Manaibu waziri wengine ni Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb) Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb) Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb) Naibu Waziri (Nishati)
Taarifa kutoka kwa mh Rais Kikwete inaeleza kutokuwa na mabadiliko yoyote katika ofisi ya rais, ofisi ya Waziri Mkuu, wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, wizara ya usirikiano wa afrika mashariki, wizara ya ujenzi, wizara ya kazi na ajira, wizara ya mawasiliano na teknolojia na wizara ya uchukuzi.
0 comments:
Chapisha Maoni