LICHA ya umri kumtupa mkono, mkongwe wa sanaa ya maigizo Bongo, Fatuma
Makongoro ‘Bi. Mwenda’ amewastaajabisha mashabiki wake baada ya kunaswa
akiwa amebandika kope za bandia.
Tukio hilo lilijiri juzikati jijini Dar wakati staa huyo alipokuwa
katika harakati za hapa na pale ndipo paparazi wetu alipomshtukia na
kumtandika picha kadhaa kisha kumuuliza, kulikoni?
“Hahaha! Jamani hebu mniache kidogo na mimi nataka niende na wakati
kwanza ni vigumu kunibaini kama nimeweka kope hizi hasa ukiwa siyo
mfuatiliaji wa mambo haya,” alisema Bi. Mwenda.
0 comments:
Chapisha Maoni