Mwanamama mkongwe katika tasnia ya filamu Tanzania, Salma Salmin 'Sandra' ameeleza kuwa kikubwa kinachoikwamisha tasnia hiyo ambayo kwa mwenyekiti wake ni Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ni watu kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kwa kuwa labda wanatoka kimapenzi au kutegemea kupewa rushwa ya ngono ili impe shavu mtu.
“Namsihi sana huyu kiongozi wetu wa sasa awe makini na hili suala, yeye pamoja na utawala wake wote wapinge haya mambo na tushikamane ile kuleta maendeleo, maana kila siku wanaopewa madili ya maana ni walewale lakini wengine tunaheshimika kwa majina tu huku dhiki zikitutawala,” alisema Sandra.
0 comments:
Chapisha Maoni