Miaka 112 iliyopita sawa na tarehe 12 Disemba mwaka 1901, kwa mara ya
kwanza katika historia ya mwanadamu, kulifanyika mawasiliano ya kwanza
ya maneno kutoka eneo moja hadi eneo jingine huko Italia kupitia mawimbi
ya radio na bila ya kutumiwa waya, hatua ambayo ilifungua ukurasa mpya
katika sekta ya mawasiliano. Mbunifu wa transimita na chombo
kilichotumika katika kuunganisha mawasiliano hayo alijulikana kwa jina
la Gugliemo Marconi, mwanafizikia wa Italia. Baadaye Marconi alifanikiwa
pia kuvumbua radio.



0 comments:
Chapisha Maoni