Leo ni Alkhamisi tarehe 9 Safar 1435 Hijria sawa na Disemba 12, 2012.
Siku kama hii ya leo miaka 50 iliyopita Kenya ilipata uhuru kutoka
Uingereza.
Kenya ilivamiwa na kukaliwa kwa mabavu mwanzoni mwa karne ya
20 na mwaka 1920, nchi hiyo iliwekwa rasmi chini ya mkoloni Mwingereza.
Sambamba na kukoloniwa nchi hiyo, Wakenya walianzisha harakati ya
wananchi ya kupigania uhuru na kujikomboa chini ya uongozi wa Jomo
Kenyata.
Wazalendo wa Kenya walipata viti vingi vya uwakilishi katika
Baraza la Kutunga Katiba katika uchaguzi uliofanyika mwezi Februari
mwaka 1961.
Hatimaye Kenya ilijipatia uhuru katika siku kama hii ya leo
na mwaka mmoja baadaye nchi hiyo ikaanzisha mfumo wa jamhuri chini ya
uongozi wa Jomo Kenyatta.




0 comments:
Chapisha Maoni