Imeelezwa kuwa watu wanaotumia redio za simu wako hatarini kupatwa na
ugonjwa wa saratani ya sikio na kichwa kutokana na mionzi mikali
itokanayo na viselula hivyo.
Akizungumza na FICHUO TZ, Dk.
Leopard Mwinuka alisema, watakaoathirika na tatizo hilo ni wanaotumia
muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikioni
‘headphone’.
“Nawaonea
huruma wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia
spika za masikio, kwani madhara yake hawawezi kuyaona sasa bali siku
zijazo watapata ugonjwa wa saratani,” alisema Dk. Mwinuka.
Alimaliza kwa kusema kuwa, mbali na kupata ugonjwa huo, wahusika
wanaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri kwa sababu, mtu anapotumia
spika za sikio huweka sauti kubwa ili apate mdundo mzuri baada ya muda
ngoma ya sikio inaathiriwa na hali hiyo.
Habari nyingine za kitabibu zilisema kwamba, kwa kuwa pande zote za
spika zina sumaku, huweza kuvutana na kuvuruga mpangilio wa ubongo hasa
kama spika hizo zitakaa maskioni kwa zaidi ya saa nne.



0 comments:
Chapisha Maoni