Mtindo wa maisha unawafanya wengi kutumia magari au usafiri wa aina nyingine hata katika eneo la umbali mfupi.
Kama wazee wetu walivyoishi kwa kutembea hata sisi
tunajionea jinsi walivyo wakakamavu na walivyoishi muda mrefu. Miongoni
mwa mazoezi mepesi na yasiyo na masharti makubwa ni yale ya kutembea.
Kutembea ni njia rahisi za kufanya mazoezi.
Huhitaji vipimo vya afya kuweza kufanya zoezi hili na badala yake unahitaji mavazi yasiyokwaza, pamoja na mahali pa kutembelea.
Wakati wataalamu wa afya wanapendekeza kupata
ushauri wa daktari kabla ya kuanza kufanya mazoezi magumu, lakini
mazoezi mepesi yanashauriwa kwa mtu yeyote na mahali popote.
Wataalam wa masuala ya afya, wanasema kutembea ni
njia salama na nzuri inayosaidia kuujenga na kuuimarisha moyo uwe na
afya nzuri na usio katika hatari ya kushambuliwa na maradhi. Kiongozi wa
mazoezi katika Gym ya ‘Fitness Mobb’ Sinza , Zakaria Malya anasema
mazoezi au tabia ya kufanya mazoezi inayo faida kubwa zaidi kuliko
matumizi ya dawa.
Kutembea ni moja ya mazoezi yanayohimizwa kufanya na yanayoweza kusaidia kujenga afya ya mwili.
Wataalamu wa masuala ya afya na magonjwa ya moyo
wanasema kutembea ni miongoni mwa kinga ya mwili kushambuliwa na
magonjwa mbalimbali ukiwemo wa moyo na kiharusi.
Kutembea vile vile ni tiba kwa mtu mwenye
kusumbuliwa na matatizo ya ubongo na kwamba, badala ya kujenga tabia ya
kutumia dawa za kupunguza msongo wa mawazo, ni vyema mtu mwenye tatizo
hilo akajenga tabia ya kutembea kwa dakika 20-30 kila siku.
Kutembea kunazuia ugonjwa wa kisukari kutokana na mazoezi hayo kuboresha uwezo wa mwili wa kutumia tezi ya insulini.
Kutembea vilevile kunaiweka mifupa kuwa imara na
kuikinga na mashambulizi ya kuzuia ugonjwa wa mifupa. Kutembea
kunasaidia kupunguza uzito unaoongezeka bila mpangilio.




0 comments:
Chapisha Maoni