Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limefungia mashindano ya Miss Utalii Tanzania kwa muda usiojulikana kuanzia Oktoba 10, 2013.
Akitangaza taarifa hiyo kwa niaba ya Kaimu Katibu
Mtendaji, Ofisa Habari Mkuu wa Basata, Agnes Kimwaga alisema uamuzi huo
umetokana na waandaaji wa mashindano hayo kukiuka masharti, kanuni
miongozo na taratibu za uendeshaji mashindano ya urembo kama ilivyowekwa
na Serikali.
Alisema pia waandaaji hao walishidwa kufanya
tathimini ya mashindano ya Misis Utalii 2012/13 kwa muda uliokubalika
baada ya mashindano pamoja na Basata kuwakumbusha kufanya hivyo.
“Uamuzi huu umefikiwa baada ya kupatikana kwa
ushahidi wa kutosha kutoka kwa warembo wenyewe juu ya unyanyaswaji wa
kijinsia kwa washiriki, ikiwemo wale waliojihusisha kimapenzi na
viongozi wa juu wa mashindano ili kupewa ushindi,” alidai Agnes.
Akizungumzia suala hilo, Rais wa Miss Utalii
Tanzania, Gideon Chipengaulo alisema ni kweli wamepokea uamuzi wa Basata
lakini sababu walizoelezwa kusimamishwa ni kuweka kambi kwa muda mrefu,
kutokukamilisha tathimini kwa wakati na kuhamisha sehemu ya mashindano.
Alisema uamuzi huo wa Basata hauichukulii kama
adhabu, kwani Bodi ya Miss Utalii Tanzania ilishaamua kusimamisha
mashindano hayo kwa msimu wa mwaka mmoja tangu Agosti 2013 baada ya
kugundua kasoro mbalimbali ikiwemo hujuma kutoka kwa baadhi ya wajumbe
na washiriki.
“Katika kipindi cha miaka mitano tuliyoendesha
mashindano, kumekuwepo na hujuma nyingi ikiwemo kupandikizwa kwa
washiriki na baadhi ya wajumbe wa bodi waliokuwa na lengo la kuharibu
mashindano,” alidai Chipungahelo.



0 comments:
Chapisha Maoni