Jumatano, Novemba 06, 2013

MKUTANO WA MAZINGIRA KUKUTANA NCHINI KENYA

Wakurugenzi watendaji kutoka nchi tofauti duniani leo wanatarajiwa kukutana nchini Kenya katika mkutano unaofanyika kwa lengo la kuwekwa mkakati wa kimataifa wa kukabiliana na jinai za mazingira.
Ripoti kutoka Nairobi zinaeleza kuwa, mkutano huo wa siku 3 umeandaliwa na Mpango wa Mazingira wa Kimataifa kwa ushirikiano na Polisi ya Kimataifa (Interpol) na mada kuu yake ni kuongezwa ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali na kuchukuliwa hatua za pamoja ili kukabiliana kimataifa na jinai za kimazingira.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na waratibu wa mkutano huo hapo jana imeeleza kuwa, Intepol na Mpango wa Mazingira wa Kimataifa zimefahamu kuwa ushirikiano ndio njia pekee ya kufanikisha malengo ya taasisi na mashirika mbalimbali ya maliasili, mazingira na viumbe hai na kukabiliana na wanaovunja sheria za  mazingira.

0 comments:

Chapisha Maoni