Siku kama ya leo miaka 1374
iliyopita yaani tarehe Pili Muharram mwaka 61 Hijria Imam Hussein AS
mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) akiwa pamoja na familia yake waliwasili
katika ardhi ya Karbala katika Iraq ya leo. Miezi kadhaa kabla ya hapo,
Imam Hussein AS aliondoka katika mji wa Madina na kuelekea Makka
akilalamikia utawala wa kimabavu wa Yazid bin Muawiya na baadaye
akaelekea katika mji wa Kufa huko Iraq. Japokuwa watu wa Kufa mwanzoni
waliunga mkono mapambano ya Imam Hussein na kumualika katika mji huo,
lakini waliacha kumuunga mkono mjukuu huyo wa Mtume wa Uislamu kutokana
na kuhofia utawala wa Yazid na vilevile ahadi nyingi za urongo za
mtawala wa Kufa.
Tarehe 6 Novemba 1860 Abraham
Lincoln aliyekuwa mpinzani wa utumwa nchini Marekani, alichukua madaraka
na kuwa rais wa nchi hiyo. Katika kipindi cha uongozi wake vita kadhaa
vilitokea nchini humo na kupelekea waliokuwa wakiunga mkono utumwa
kushindwa. Abraham Lincoln aliuawa mwaka 1865 na mmoja wa wapinzani wa
harakati za kupinga utumwa nchini Marekani.
Na siku kama ya leo miaka 35
iliyopita inayosadifiana na tarehe 15 Aban 1357 Hijria Shamsia, ulianza
mgomo wa wafanyakazi wa Shirika la Redio na Televisheni ya Iran kwa
lengo la kuushinikiza utawala wa Shah uondoke madarakani. Siku hiyo hiyo
maafisa wa usalama wa Shah walivamia taasisi za magazeti na kuwakamata
baadhi ya waandishi habari suala lililopelekea magazeti maarufu
kusimamisha uchapishaji wake.




0 comments:
Chapisha Maoni