Serikali ya Ethiopia imeweka tayari askari wake wa usalama na
polisi ili kukabiliana na mashambulizi yanayoweza kufanywa na kundi la
as Shabab.
Taarifa rasmi ya serikali ya Addis Ababa imeeleza kuwa,
wamepokea ushahidi kwamba kundi la as Shabab linaweza kushambulia nchi
hiyo na kwa ajili hiyo askari wake wa usalama na polisi wameandaliwa
kikamilifu.
Hayo yanajiri katika hali ambayo wiki 3 zilizopita Wasomali
wawili waliokuwa wamejifunga mabomu walijilipua kati ya watazamaji wa
mpira wa miguu wakati wa mechi kati ya Ethiopia na Nigeria. Kundi la as
Shabab limesema kuwa, litashambulia nchi ya Ethiopia ili kulipiza kisasi
cha kupelekwa wanajeshi wa nchi hiyo katika ardhi ya Somalia.
Vyombo vya usalama na upelelezi vya Ethiopia vimetangaza kuwa, kuna
ushahidi unaoonesha kuwa, kundi la as Shabab linaungwa mkono na Eritrea
ili kushambulia mji wa Addis Ababa na maeneo mengine ya Ethiopia.



0 comments:
Chapisha Maoni