Maghorofa
64 yaliyopo eneo la Kariakoo, Manispaa ya Ilala yamejengwa kinyume na sheria na
kwamba baadhi yanaweza kuporomoka kutokana na ujenzi wake kuwa chini ya
kiwango.
Kampuni iliyopewa zabuni ya kufanya ukaguzi wa majengo Manispaa ya
Ilala, inayoitwa Design Plus Architects (DPA) imebaini kati ya majengo ya
ghorofa 90 yaliyokaguliwa, 67 yamejengwa kinyume na sheria.
Uamuzi wa kuipa kampuni binafsi kazi ya kukagua majengo, umekuja
baada ya jengo la ghorofa 16 kuanguka na kuua watu 36 Machi 26, mwaka huu.
Meneja Uendeshaji wa DPA, Mustafa Maulid amesema kwamba ukaguzi wa
majengo hayo umeanza Julai mwaka huu baada ya kupata zabuni hiyo.
Maulidi amsema kuwa hali ni mbaya katika majengo waliyoyakagua,
kuna majengo ya ghorofa yenye nyufa nyingi, pia yapo majengo yanayogusana
ambayo ni hatari kwa watumiaji.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alipoulizwa hatua za
kuchukua, amesema vikao vya madiwani vitaamua hatua za kuchukua baada ya
kuipitia ripoti ya ukaguzi huo.
Akifafanua zaidi, Maulid amesema makosa waliyoyabaini ni watu
kuendesha ujenzi bila kuwa na vibali.
Aidha amesema kuwa makosa mengine ni ujenzi bila kufuata michoro
iliyoidhinishwa na Manispaa ya Ilala.



0 comments:
Chapisha Maoni