Jumatano, Agosti 28, 2013

WAMAREKANI WAADHIMISHA MIAKA 52 YA "I HAVE A DREAM" YA MARTIN LUTHER KING

Wamarekani wanaadhimisha miaka 52 tangu maandamano ya kuelekea Washington na hotuba ya kihistoria “I Have a Dream” iliyotolewa na mchungaji Martin Luther King mbele ya makumbusho ya Rais Lincoln. 
Tangu jumamosi maelfu ya Wamarekani wamekuwa wakiwasili katika mji mkuu wa Marekani kuhudhuria sherehe mbali mbali zilizoandaliwa ili kukumbuka siku hii muhimu ya Agosti 28 iliyobadili kabisa ukurasa wa historia na haki za kiraia Marekani.

Siku ya Jumamosi maelfu na maelfu ya wamarekani waliwasili kutoka pembe mbali mbali za nchi hii ili kuiga maandamano yaliyofanyika miaka 50 kumkumbuka kiongozi wa kutetea haki za kiraia aliyeuliwa pamoja na kuwasilisha ujumbe sawa na uliyotolewa wakati ule kuhusiana na maswala mbali mbali ya kijamii.

Watayarishaji na waandamanaji wametoa wito kutaka kutekelezwa maswala mbali mbali, ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuanzia haki za wanawake na raia, hadi mageuzi ya uhamiaji, kukomeshwa ghasia za bunduki na kubuniwa nafasi za ajira.

0 comments:

Chapisha Maoni