Jumatano, Agosti 28, 2013

AKAMATWA NA KILOGRAMU 30 ZA NYAMA YA SIMBA MBEYA

Mtu mmoja amekamatwa na nyama ya simba kiasi cha kilogramu 30 katika hifadhi ya taifa ya Ruaha wilayani Mbalali mkoani Mbeya jana saa 12:30 asubuhi.


Habari toka kwa maafisa wa polisi zinaeleza kuwa makachero wa polisi wamemkamata FRED KALINGA, 24, Mhehe, Mkulima na mkazi wa kijiji cha Kwatanga akiwa na nyara za serikali nyama ya samba kilogramu 30 ndani ya hifadhi hiyo.

Habari zinasema kuwa mtuhumiwa alitumia mbinu ya kupakia nyama hiyo katika pikipiki yake yenye namba za usajili T.387 AZA aina ya SUNLG na pia imeelezwa kuwa mtuhumiwa ni muwindaji haramu. Taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani.

Naye Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, kamishna msaidizi wa polisi Diwani Athumani anatoa wito kwa jamii kuacha mara moja kujihusisha na ujangili kwani ni kinyume cha sheria na kwamba msako mkali utaendelea kufanywa na vyombo vyote vya ulinzi na usalama.

Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa juu ya mtu au watu wanaomiliki nyara za serikali au wawindaji haramu azitoe katika mamlaka husika ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe mara moja.

0 comments:

Chapisha Maoni