Jumamosi, Agosti 10, 2013

OLE WAKE ASAFIRISHAYE WAKIMBIZI

Polisi wa Uspania wanasema kwamba wamelikamata gengi linalosafirisha wahamiaji kimagendo.
 
Watu 75 wametiwa mbaroni Uspania na Ufaransa. Msemaji alieleza kuwa gengi hilo likiwasafirisha raia wa Uchina na kuwaingiza kimagendo katika nchi za Ulaya na Marekani, na kila mkimbizi akilipa kama Euro 50,000 kwa safari hiyo.
Polisi wanasema viongozi wa gengi hilo Ulaya waliokuwa na makao yao mjini Barcelona, ni kati ya wale waliokamatwa.
Polisi piya wamekuta paspoti zaidi ya 80 za nchi kama Japan, Hong Kong na Singapore.

0 comments:

Chapisha Maoni