Jumamosi, Agosti 10, 2013

MASHINDANO YA RIADHA YAMEFUNGULIWA LEO MOSCOW, URUSI

Mashindano ya Riadha ulimwenguni yamefunguliwa hii leo mjini Moscow nchini Urusi.

Haya ndio ya mwanzo kati ya mashindano matatu yatayofanywa Urusi katika miaka mitano ijayo, pamoja na Olimpiki za Winter na Kombe la Kandanda la Dunia la mwaka 2018.
Mbio za kwanza za mashindano hayo zitajumuisha wanariadha mashuhuri kama vile bingwa wa mbio za mita 100 Usain Bolt na mshindi mara mbili wa mbio za Olympiki raia wa uingereza Mo Farah.
Matayarisho ya mashindano hayo hata hivyo yamekumbwa na kashfa za baadhi ya wanariadha wanaotumia dawa za kuzidisha nguvu, huku waandalizi wakisema kuwa watatumia ukaguzi maalum wa kuwazuia wanariadha watakaotumia dawa hizo.

0 comments:

Chapisha Maoni