Jumamosi, Agosti 10, 2013

MILIONI 100 KUTUMIKA KATIKA MAZISHI YA BILIONEA ALIYEUAWA ARUSHA

Zaidi ya Sh100 milioni zinatarajiwa kutumika kugharimia mazishi ya mfanyabiashara, bilionea wa madini ya Tanzanite, Erasto Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi 21 Jumatano ya Agosti 7, mwaka huu.

Kiasi hicho kinachotarajiwa kuchangwa na wafanyabiashara wenzake wa madini kitatumika pia kulipia gharama za magari maalumu yatakayotumika kwenye msafara wa mazishi ya Msuya yanayotarajiwa kufanyika nyumbani kwao Mirerani, wilayani Simanjiro.
Habari kutoka kamati ya mazishi inayoundwa na wafanyabiashara wa Tanzanite, ikiongozwa na kaka mkubwa marehemu Msuya, Gady Msuya, gari maalumu la kubeba mwili wa marehemu na jeneza vimeagizwa kutoka Nairobi, nchini Kenya kwa gharama ya Sh8 milioni.

0 comments:

Chapisha Maoni