Jumamosi, Agosti 10, 2013

MAREKANI KUPUNGUZA UCHUNGUZI WA MAWASILIANO

Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza mipango ya kupunguza uchunguzi wa mawasiliano ya umma na serikali, wiki chache baada ya mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani, Edward Snowden kufichua siri.


 
Edward Snowden
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ikulu ya Marekani jana Ijumaa (09.08.2013), Rais Obama amesema kuwa mipango hiyo inaandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watu wa Marekani wanakuwa na imani na juhudi zinazofanywa na serikali yakiwemo mashirika ya kijasusi.
Rais Obama ameuambia ulimwengu kwamba Marekani haina nia ya kuwafuatilia watu wa kawaida.
Amesema ataliomba bunge kufanyia mageuzi moja ya ibara ya sheria ya uzalendo iliyopitishwa baada ya mashambulizi ya Septemba 11, mwaka 2001 kifungu namba 215, ambacho kinaipa serikali uwezo wa kusikiliza mawasiliano ya simu pamoja na kukusanya data nyingine za raia wake.

0 comments:

Chapisha Maoni