Jumapili, Machi 05, 2017

NI TRUMP NA OBAMA TENA!!!

Rais wa Marekani Donald Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter hapo jana, alimshutumu mtangulizi wake Barack Obama kwa kutega simu za ofisi yake iliyoko katika jengo la Trump Tower, New York wakati wa kampeini za urais. 
Madai hayo ya Trump yanakuja huku utawala wake ukikabiliwa na maswali kuhusu wanachama wa kundi lake la kampeini kuwasiliana na Urusi kabla ya kuapishwa kwake kama Rais wa Marekani.
Hotuba ya kwanza ya kiongozi huyo mpya wa Marekani bungeni wiki hii iligubikwa na ufichuzi kuwa mwanasheria mkuu Jeff Sessions alikutana mara mbili na balozi wa Urusi nchini Marekani jambo ambalo hakulifichua kabla ya kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu. 
Mashirika ya ujasusi ya Marekani yamesema ushawishi wa Urusi ulimsaidia Trump kushinda uchaguzi.

0 comments:

Chapisha Maoni