Jumatano, Machi 01, 2017

USHOGA MFUPA MGUMU KWA KIGWANGALLA?

Tanzania imerudi nyuma katika uamuzi wake wa hapo awali wa kutangaza hadharani majina ya mashoga wanaouza huduma za ngono kwenye mitandao ikisema kuwa hatua hiyo huenda ikaharibu ushahidi dhidi ya washukiwa hao.
Naibu waziri wa afya Hamisi Kigwangalla alisema kuwa serikali itashughulikia swala hilo na kutoa taarifa kwa umma baadaye. 
Awali Kigwangalla aliratibiwa kutoa orodha ya mashoga wanaouza huduma za ngono mitandaoni katika mkutano wake na waandishi wa habari siku ya Jumatatu. 
Kigwangalla alisema kutangaza majina ya washukiwa hao ni kama “kufungulia shetani ambaye tayari amewekwa ndani ya chupa”.

0 comments:

Chapisha Maoni