Ombi la mtandao la kumtaka Barrack Obama kuwania urais katika uchaguzi mkuu nchini Ufaransa limewavutia takriban wafuasi 42,000.
Mabango ya kampeni yanayosomeka ''Oui, on Peut'' ikimaanisha kauli mbiu ya kmpeni ya Obama ''Yes we can'' yametumika mjini Paris.
Bwana Obama sio raia wa Ufaransa hivyobasi hawezi kugombea urais.
Lakini wale wanaofanya mzaha huo wanasema kuwa lengo lao ni kuonyesha kwamba hakuna wagombea wazuri .
Ujumbe wao kwa wagombea hao kama alivyosema mmoja ya waandalizi wa ombi hilo ni ''jamani hamufai'.
Wapiga kura wa Ufaransa watashiriki katika uchaguzi mkuu mnamo tarehe 25 mwezi Aprili na iwapo wagombea hawatapata asilimia 50 ya kura katika raundi ya kwanza basi wapiga kura watarudi tena mnamo tarehe 7 mwezi Mei ili kuamua kati ya wagombea wawili waliopata kura nyingi.
Mgombea mwenye umaarufu katika uchaguzi huo ni Marine Le Pen ambaye amenufaiki na shutuma zinazomkabili mpinzani wake Francois Fillon tangu mwezi Januari hatua iliomfanya hakimu mmoja kusema kuwa ataanzisha uchunguzi kuhusu madai hayo.
Kura mbili za maoni zinamuonyesha Marine Le pen akiongeza dhidi ya Fillion lakini inasemekana kwamba wapinzani wake wanaweza kumshinda iwapo itafikia awamu ya pili ya uchaguzi.
0 comments:
Chapisha Maoni